Posts

MADA YA KWANZA: MAWASILIANO

  SOMO LA:  KISWAHILI KIDATO:  CHA KWANZA                              MADA YA  KWANZA: MAWASILIANO Katika mada hii unatarajiwa kuelewa fasili ya mawasiliano na jinsi mchakato wa mawasiliano unavyofanyika. Utaelewa dhana ya lugha na vipengele muhimu vinavyokamilisha fasili ya lugha. Utaelewa dhima kuu za lugha, matumizi na umuhimu wake. Vilevile katika mada hii utajifunza juu ya lafudhi na matamshi mbalimbali ya watumiaji wa lugha ya Kiswahili. Lugha kama Chombo cha Mawasiliano Mawasiliano ni mchakato wa kuhawilisha taarifa kwa njia ya ubadilishanaji wa mawazo, hisia, malengo, tabia, matarajio, mitazamo kupitia mazungumzo, ishara na maandishi. Ni ubadilishanaji wa taarifa unaoleta maana baina ya pande mbili au zaidi ambazo zinaweza kuwa viumbe hai au kinyume chake. Sasa hapa sisi tutajikita katika mawasiliano yanayofanywa baina y...

MADA YA PILI : AINA ZA MANENO

   MADA YA PILI: AINA ZA MANENO Katika lugha ya Kiswahili kuna angalau aina nane za maneno ambazo wataalamu wengi wa lugha wanakubaliana hivyo. Katika mada hii utaweza kujifunza na kubainisha aina zote nane za maneno na jinsi zinvyotumika katika sentensi. Utaweza pia kujifunza namna ya kutofautisha aina za maneno ambazo zimeleta ubishi miongoni mwa wataalamu wengi hususani katika Viunganishi na Vihusishi. Ubainishaji wa aina Saba za Maneno Aina Saba za Maneno ya Kiswahili Bainisha aina saba za maneno ya Kiswahili Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili ni pamoja na hizi zifuatazo: Nomino (N) Viwakilishi (W) Vitenzi (T) Vivumishi (V) Vielezi (E) Viunganishi (U) Vihusishi (H) Vihisishi (I) Ufafanuzi wa aina za Maneno Nomino (N) Nomino ni maneno yanayotaja vitu, watu, na hali kadhalika. Kuna aina mbali mbali za maneno ambazo ni pamoja na hizi zifuatazo: Nomino za pekee: Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si kingi...